Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Visa Application Centre

Kituo cha Maombi ya Viza ni nini (Kituo cha Maombi ya Viza za Kanada)

Vituo vya Maombi ya Viza za Kanada vimeanzishwa ili kutoa msaada wa kiutawala kwa wateja kwaajili ya kufanikisha kuwasilisha maombi ya viza za muda mfupi (viza za matembezi, vibali vya masomo na kazi) pamoja na hati za kusafiria kwa wakazi wa kudumu wa Kanada katika ofisi za IRCC duniani kote.

Ni nani aliye na mkataba na Kituo cha Maomb ya Viza za Kanada nchini Tanzania?

VFS Global ni kampuni binafsi iliyopewa kibali na IRCC kuendesha Kituo cha Maombi ya Viza za Kanada nchini Tanzania.

Nimesikia kwamba kutakuwa na mkataba tofauti kuanzia tarehe 02 Novemba 2019. Mkataba huo utaniathiri vipi?

Tafadhali tembelea www.Canada.ca/immigration kwa taarifa zaidi kuhusu mahitaji mapya na huduma mpya za mkataba.

Je niwasilishe maombi yangu ya viza mapema, au nisubiri kidogo?

Tafadhali zingatia kuwa miongozo yote kuhusina na muda wa mchakato wa maombi ya viza, tarehe za safari, pamoja na mambo mengine yatabaki kama yalivyo. Tafadhali tembelea www.Canada.ca/immigration kwa taarifa zaidi kuhusu mabadiliko ambayo yataanza kutumika rasmi tarehe 02 Novemba 2019 ili uamue lini uwasilishe maombi yako.

Nini kitatokea kama maombi yangu hayatarudishwa Kituo cha Maombi ya Viza mpaka kufikia tarehe 01 Februari 2020?

Kama uliwasilisha maombi yako katika Kituo cha Maombi ya Viza siku ya tarehe 01 Novemba 2019 au kabla ya hapo, office ya IRCC itaratibu urudishaji wa nyaraka.

Nimeona kwamba gharama za kurudisha pasipoti zimeongezeka. Je nitatakiwa kulipia tofauti ya kiasi kilichoongezeka kama pasipoti yangu itarudishwa baada ya tarehe 01 Novemba 2019?

Huduma zote zilizolipiwa kabla ya tarehe 02 Novemba 2019 zinahesabika kama zimekamilika kimalipo.

Je ninaweza kuweka miadi ya dharura?

Waombaji wanaoomba miadi ya dharura kwaajili ya biometriki wanaweza kuomba miadi hiyo ikiwa tu wataonesha uthibitisho unaoridhisha wa dharura wafikapo kwenye miadi. Uthibitisho halali unaweza kuwa barua/nyaraka kutoka kwa ofisi. Tafadhali elewa kwamba uthibitisho huo wa dharura unatakiwa kuoneshwa tu katika Kituo cha Maombi ya Viza na sio kukusanywa pamoja na maombi yako, na uthibitisho huo utakuwezesha kuweka miadi ya dharura kwaajili ya biometriki lakini hautaathiri muda wa IRCC kushughulikia ombi lako. Kwa maelezo Zaidi au maswali, Kituo cha Huduma kwa Wateja kinaweza kutoa msaada wa maulizo yoyote.

Tafadhali bofya hapa Kuweka Miadi

 

Mchakato wa Maombi ya Viza

Niwasilishe wapi maombi yangu ya viza?

Unaweza kuwasilisha maombi yako ya viza katika Kituo cha Maombi ya Viza za Kanada. Maombi yanaweza pia kuwasilishwa kwenda ofisi za IRCC kwa kutumia mfumo wa kimtandao wa maombi ya viza wa IRCC(E-Apps)

 

Je mtu mwingine anaweza kuwasilisha maombi kwa niaba yangu?

Unaweza kuteua muwakilishi akuwasilishie maombi kwa niaba yako. Ili kufanya hivyo, tafadhali jaza Fomu ya Kutumia Uwakilishi na/ au Fomu ya Ridhaa ya VFS Global, kumruhusu muwakilishi awasilishe au achukue kifulushi cha maombi yako/ bahasha yenye majibu kwa niaba yako.

 

Je nitatakiwa kwenda mwenyewe kutoa alama za vidole na picha kila ninapofanya maombi ya viza?

Kama unawasilisha maombi ya viza kwaajili ya makazi ya muda mfupi, masomo na/au vibali vya kufanya kazi na unahitajika kutoa alama za vidole na picha, unatakiwa kutoa biometriki kwa mara moja ndani ya miaka 10.

Kama unawasilisha maombi ya makazi ya kudumu, na unahitajika kutoa biometriki, unapaswa kutoa biometric kila unapowasilisha maombi.

Ili kujua kama unahitajika kutoa biometriki, tafadhali tembelea http://www.cic.gc.ca/english/visit/biometric.asp.

 

Mara ninapotoa alama za vidole na picha, alama zangu za vidole zitakuwa halali kwa muda gani?

Kuanzia Julai 31, 2018, biometriki zinadumu kwa miaka kumi. Kama umetoa alama zako za vidole na picha zamani, zitaendelea kutumika kwa miaka kumi tangia siku zilipochukuliwa. Muda wa matumizi ya Viza au kibali hauwezi kuzidi muda wa matumizi ya alama zako za vidole na picha. Waombaji wa Makazi ya Kudumu watatakiwa kutoa alama za vidole na picha kila wanapowasilisha maombi.

Alama zako za vidole zitafutwa moja kwa moja kama utapewa Uraia wa Kanada ndani ya kipindi cha miaka 10.

 

Je natakiwa kutoa buometriki kwa ajili ya maombi yangu ya viza?

 Ili kujua kama unahitajika kutoa biometriki, tafadhali tembelea http://www.cic.gc.ca/english/visit/biometric.asp.

 

Je ni lazima niweke miadi kwajili ya kutoa alama zangu za vidole na picha katika Kituo cha Maombi ya Viza za Kanada?

Kuanzia tarehe 02 Novemba 2019, ni lazima kuweka miadi kwa ajilia ya kufanya bayometriki kwenye Kituo cha Maombi ya Viza za Kanada nchini Tanzania.

 Ili kujua kama unahitajika kutoa biometriki, tafadhali tembelea http://www.cic.gc.ca/english/visit/biometric.asp.

Tafadhali tambua kwamba, kwaajili tu ya kupanga miadi, VFS Global itachukua taarifa binafsi toka kwa mteja. Fomu ya ridhaa kwa ajili hiyo itatakiwa toka kwa mwombaji wa viza.

 

Nitalipiaje ada za Serikali ya Kanada kwaajili ya maombi yangu ya viza?

Ada za Serikali ya Kanada zinaweza kulipwa mtandaoni kupitia tovuti ya IRCC kwa kadi ya malipo au mkopo kutokea Benki ya kikanada kwa kutumia INTERAC® Online na zilizosajiliwa kufanya malipo ya mtandaoni kupitia tovuti ya benki. Kulipia ada za serikali ya Kanada mtandaoni tafadhali bofya hapa

 

Nitalipiaje ada za huduma za Kituo cha Maombi ya Viza?

Maelekezo ya malipo kwa ajili ya ada za huduma za Kituo cha maombi ya Viza:

 Kwa maelekezo kamili kuhusiana na ulipaji wa ada za Serikali ya Kanada na ada za huduma za Kituo cha Maombi ya Viza za Kanada tafadhali bofya hapa

 

Nini kitatokea nikiisha wasilisha maombi yangu ya viza?

Ukishawasilisha maombi yako katika Kituo cha Maombi ya Viza, mfanyakazi wa Kituo cha Maombi ya Viza atakagua ukamilifu wa maombi yako kulingana na vigezo vya IRCC na watawaslisha maombi yako kwa niaba yako siku ya kazi inayofuata.

Mara maamuzi juu ya maombi yako yakiishafanywa, ofisi za viza zitarudisha kwa usalama pasipoti yako kwa katika Kituo cha Maombi ya Viza, ambao watakutaarifu kwa njia ya mawasiliano utakayoipendelea wewe. Taarifa itatolewa pia katika Mfumo wa Ufuatiliaji wa Maombi Mtandaoni, kukujulisha kwamba majibu ya maombi yako yapo tayari kurejeshwa. Majibu ya maombi yako yatarudishwa kwako kwa njia ya urejeshaji utakayopendelea.

 

Ninahitaji Viza ya aina gani?

Aina ya viza unayohitaji itategemea na dhumuni la safari yako ya Kanada. kwa taarifa zaidi kuhusu aina za viza tafadhali angalia taarifa za kina zilizomo katika tovuti IRCC

 

Nianawezaje kufuatilia maendeleo ya maombi yangu?

Maendeleo ya maombi yako yanaweza kufuatiliwa kwa urahisi kwa kubofya “Fuatilia Maombi yako”

 

Ninawezaje kuipata pasipoti yangu?

Kupata pasipoti yako (zako), una machaguo mawili:

1. Kuchukua pasipoti yakow ewe mwenyewe toka Kituo cha Maombi ya Viza au,

2. Kuomba pasipoti yako irudishwe kwa njia ya kuria

Tafadhali tambua kuwa kutakuwa na ada za huduma tajwa hapo juu. Ada za Kuria zinapohusika ni tofauti na ada za malipo kwaajili ya Huduma za Kuwasilisha Pasipoti. Taarifa zaidi zinaweza kupatikana katika ukurasa wa ada za huduma.

 

Ninahitaji kuwa na nyaraka gani ili niweze kupata pasipoti yangu?

Kama unachukua paspoti yako wewe mwenyewe, ni lazima uje na:

1. Nakala ya ukurasa wenye picha wa pasipoti yako uliopigwa muhuri.

2. Risiti halisi iliyotolewa na Kituo cha Maombi ya Viza

3. Kitambulisho cha kiserikali

 

Mchakato wa viza utachukua muda gani?

Kwa muda wa mchakato wa maombi wa hivi karibuni, tafadhali tembelea tovuti ya Ofisi ya Viza

 

Je nitatakiwa kuhudhuria kwenye usahili katika Ofisi za Viza?

Immigration, Refugees and Citizenship Canada may require you to attend an interview at the Visa Office. The Visa Application Centre will contact you, or you might be contacted directly by the Visa Office and you will also be notified by an update on the Online Application Tracking System.

 

Niwasiliane nan ani kwa maelezo zaidi?

You may contact the call centre operated by the Visa Application Centre (please refer to the Contact Us tab on the left of this page), or alternatively visit the Immigration, Refugees and Citizenship 

 

Huduma gani za ziada zipo kwaajili yangu?

Kituo cha Maombi ya Viza kinatoa aina mbalimbali za huduma kwa manufaa yako na kurahisisha ufanyaji wa maombi ya Viza kama vile kutoa nakala (fotokopi), kuria, msaada wa kujaza fomu. Kwa maelezo kamili na gharama za huduma hizo tafadhali rejea “Orodha ya Huduma na Ada za Huduma”

 

Ninampango wa wa kwenda Kanada kusoma kwa kipindi kisichozidi miezi sita lakini ninaweza kuhitaji kuongeza muda wa masomo. Je niwasilishe aina gani ya maombi? Je niwasilishe aina gani ya maombi?

Tafadhali rejea: https://www.canada.ca/en/immigration-refugees-citizenship/services/study-canada/study-permit/eligibility.html

Nyaraka

Ninahitaji nyaraka gani kwaajili ya maombi yangu ya Viza?

Nyaraka zinazohitajika zinategemeana na dhumuni la safari yako. Tafadhali rejea kipengele cha Aina za Viza na ufuate viunganishi vinavyohusika vilivyowekwa hapo, au tembelea tovuti ya IRCC

 

Je Ofisi za Viza zinaweza kuniomba nyaraka au taarifa za ziada?

Ndio, Ofisi za Viza zinawezakukuhitaji uwasilishe nyaraka za ziada. Taarifa itawekwa kwenye Mfumo wa Ufuatiliaji Maombi Mtandaoni na itafuatiwa na taarifa kwa njia ya barua pepe kuhakikisha kwamba umepokea maelekezo na taarifa. Halafu utaombwa kuwasilisha nyaraka za ziada kwenye Kituo cha Maombi ya Viza amabo wataziwasilisha Ofisi za Viza kwa niaba yako. 

 

Ninataka kwenda Kanada kama mwanafunzi. Vigezo vya kifedha ni vipi?

Vigezo vya kifedha hutegemea na, pamoja na mambo mengine, muda unaoazimia kuwa Kanada. Tunashauri uangalie tovuti ya IRCC ili kupata maelezo ya hivi karibuni na kuhakikisha kwamba nyaraka zako zinakidhi vigezo vya kuwasilisha maombi yako katika Kituo cha Maombi ya Viza.

Kama wewe ni mwanafunzi unayekwenda kusoma Jimbo la Kwebeki, unatakiwa pia kupitia taarifa katika tovuti ya Uhamiaji Kwebeki