Tafadhali kumbuka kuwa kuanzia sasa, Kituo cha Maombi ya Visa cha Kanada jijini Kampala hakitatoa tena huduma za usafirishaji wa pasipoti kutokana na sababu za uendeshaji za IRCC. Wateja bado wanaweza kufanya miadi ya kuwasilisha biometriki zao.
Tafadhali bofya hapa kufanya miadi. Kiungo hiki kitakupeleka kwenye ukurasa wa usajili wa miadi ambayo itakuwezesha
Panga miadi
Ahirisha miadi
Futa miadi
Utatakiwa kufuata maelekezo yaliyowekwa kwenye ukurasa ili kutengeneza wasifu wa kuingia na kufanya miadi.
Tafadhali tambua;
VFS Globall itakusanya taarifa zako binafsi kwa nia ya kukufanya miadi tuu. Usiweke taarifa nyingine binafsi tofauti na zinazihitajika kwenye mfumo wa miadi mtandaoni kwenye barua pepe, usogozi wa mtandaoni, ujumbe mfupi wa simu (SMS) mawasiliano ya kielektroniki yasiyo na ulinzi. Utatakiwa ujaze kikamilifu fomu ya Ridhaa.
Barua ya Miadi itakupa taarifa kuhusu tarehe, muda na mahala pa miadi, pamoja na taarifa nyingine muhimu.
Utatakiwa kuwasili kwenye Kituo cha maombi ya viza dakika 15 kabla ya muda wako wa miadi uliopangwa.
Unaweza kubofya hapa kujua kuhusu Kanuni za usalama kwenye Kituo cha Maombi ya viza.


