Gharama za Huduma
Gharama za Huduma
Ada za Huduma Kuanzia Tarehe 01 Mei 2026
Kama ukitakiwa kuwasilisha bayometriki kama sehemu ya maombi yako ya IRCC,utalipa ada ya bayometriki kwa Serikali ya Kanada. Kulipa ada ya bayometriki ni pamoja na:
Ukusanyaji wa alama za vidole na picha ya kidijitali kwenye ofisi za VAC
Kusafirisha nyaraka zako kama vile paspoti yako, kati ya IRCC na ofisi ya VAC ulipotoa bayometriki zako
Hii inamaanisha kuwa, ikiwa umetoa bayometriki zako kwenye ofisi ya VAC, utapata huduma ya usafirishaji wa kifurushi kimoja. Hudumu hii itajumuisha kutuma nyaraka zako kutoka ofisi za VAC ambapo ulitoa bayometriki zako kwenda IRCC na kurudishwa ofisi za VAC, pindi IRCC itakapokamilisha kutoa maamuzi ya ombi lako.
Kuna baadhi ya utofauti. Soma kwa umakini ili kuona kama haya yanakuhusu wewe:
Kama umeshatumia huduma ya usafirishaji wa kifurushi kimoja, utahitaji kulipa ada ya huduma ya usafirishaji wa kifurushi ili kutuma nyaraka zozote za ziada kwenda IRCC
Ikiwa umefanya bayometriki zako katika ofisi ya VAC ya eneo moja, na kuwasilisha nyaraka zako kenye ofisi ya VAC eneo tofauti, utahitajika kulipa ada ya huduma ya usafirishaji wa kifurushi. Ada ya huduma itaondolewa ikiwa tu utawasilisha nyaraka zako katika ofisi ya VAC ambapo ulifanya bayometriki zako.
Ikiwa hauhitaji kufanya bayometriki, utahitaji kulipa ada ya huduma za usafirishaji wa kifurushi ili kutuma nyaraka zako kwenda IRCC kupitia ofisi za VAC
Viza ya Kusafiri Kupitia Kanada
Kama unasafiri kupitia Kanada ukielekea nchi tofauti, utaweza kuhitaji kutuma maombi ya viza ya kusafiri kupitia Kanada na kutoa bayometriki zako. Hatahivyo, hautalazimika kulipa ada ya bayometriki ya Serikali ya Kanada.Kwakuwa haulipi ada ya bayometriki, utatakiwa kulipa ada ya usafirishaji wa kifurushiili kutuma nyaraka zako kwenda IRCC kupitia ofisi za VAC
Huenda usihitaji visa ya kusafiri kupitia Kanada ikiwa unasafiri kwenda marekani. Tembele IRCC ili kujifunza zaidi kuhusu viza ya kusafiri kupitia Kanada na nani anayehitaji kutuma maombi: IRCC - Transit through Canada
Kuwasilisha maombi ya karatasi kwenda IRCC kupitia ofisi ya VAC:
IRCC inakubali maombi ya mtandaoni tuu kwa programu nyingi za Uhamiaji, lakini kuna tofauti fulani. Kuna wakati unaweza hata kuwasilisha maombi ya karatasi(yakiwa na au bila bayometriki) kwa IRCC kupitia VAC. Kuwasilisha maombi ya karatasi kupitia VAC kunahitajika kulipia huduma za usaidizi - Ada ya huduma ya maombi ya karatasi.
Njia za malipo
Kwa ajili ya maombi ya IRCC na bayometriki
Ada za Serikali ya Kanada kwa ajili ya maombi yako yanaweza kulipwa mtandaoni tu kupitia tovuti ya IRCC. Tambua jinsi ya kulipa ada hizi hapa:IRCC - Jinsi ya kulipa ada zako
Tambua: Huwezi kurejeshewa kiasi nusu au kamili cha ada ya serikali ya Kanada kwenye ofisi za VAC.Urejeshaji pesa unaweza kuombwa kwa kutembelea IRCC tuu na kuwasilisha ombi la kurejeshewa pesa. Pata maelezo zaidi hapa:IRCC - Omba IRCC kurejeshewa pesa
Kwa ajili ya Huduma za VAC
Kwa kibinafsi–Malipo yanapaswa kulipwa kwa akaunti ya Benki ya Shirika la Kimataifa la Uhamiaji Tanzania kulingana na maagizo hapa chini:
Kwa njia ya posta – Malipo yanapaswa kulipwa kwa akaunti ya Benki ya Shirika la Kimataifa la Uhamiaji Tanzania kulingana na maagizo hapa chini :
Jina la Akaunti: International Organization for Migration
Jina la Benki: ABSA Bank Tanzania
SWIFT: BARCTZTZ
Nambari ya Akaunti: 004-6004922
Kwa urejeshwaji wowote wa ada iliyolipwa Serikali ya Canada, tafadhali Bonyeza hapa kuomba marejesho kutoka kwa Serikali ya Canada.
Gharama za Huduma kwa huduma inayotolewa katika VAC
| Gharama ya huduma (kwa kila muombaji) | Kiasi kwa Dola ya Kanada (na kodi) | Kiasi kwa Shilingi za Kitanzania (na kodi) |
|---|---|---|
Nakala | $0.26 | 500.00 |
Uchapaji | $0.52 | 1,000.00 |
Ujumbe Mfupi wa Simu | $3.00 | 5,600.00 |
Gharama za Huduma kwa huduma inayotolewa katika VAC
| Gharama ya huduma (kwa kila muombaji) | Kiasi kwa Dola ya Kanada (na kodi) | Kiasi kwa Shilingi za Kitanzania (na kodi) |
|---|---|---|
| Kusafirisha kifurushi (kwa kila kifurushi) | $41.41 | 77,300.00 |
| Kuwasilisha malipo ya Ada za Serikali ya kanada (kwa kila muombaji) | $17.20 | 32,100.00 |
| Huduma ya kusaidiwa - fomu ya mtandaoni (eTA) | $3.00 | 5,600.00 |
| Huduma ya kusaidiwa – Maombi ya makaratasi (kwa kila ombi) | $17.62 | 32,900.00 |
| Huduma ya kusaidiwa – Kuskani (Kwa kila ukurasa) | $0.74 | 1,400.00 |
| Dawati la kujihudumia (kwa kila lisaa) | $8.84 | 16,500.00 |
| Kutoa kivuli (kwa kila ukurasa) | $0.26 | 500.00 |
| Kutoa nakala (kwa kila ukurasa) | $0.52 | 1,000.00 |
| Ujumbe mfupi wa maneno SMS (kwa kila muombaji) | $3.00 | 5,600.00 |
* Malipo ya huduma yanajumuisha ushuru wowote unaotumika na yanaweza kubadillika kulingana na taarifa ya serikali.
** Kiwango cha ubadilishaji wa CAD kinaamuliwa na serikali ya Canada.
Malipo mapya ya huduma yalianza kutumika mnamo tarehe 01 Mei 2026.
Gharama zote pamoja na ada ya kituo cha maombi ya viza, hayarudishiwi.
Tarehe ya uwasilishaji ya maombi ya kwa njia ya posta itakuwa tarehe ambayo Kituo cha Maombi cha Visa kinapokea maombi hayo. Ikiwa maombi yaliyoingia kwa njia ya posta yamepokelewa na hayakujumuisha malipo sahihi ya sasa ya huduma, mwombaji atajulishwa ili kulipa tofauti hiyo au maombi yatarudishwa kwa mwombaji.
Dawati la kujihudumia la VAC
Huenda ukalazimika kusubiri kutumia dawati la kujihudumia la VAC ikiwa kuna wageni wengi VAC. Muda wa kusubiri huweza kutofautiana.
Tafadhali leta USB flash drive yako kama unakusudia kutumia dawati la kujihudumia la VAC na uhakikishe kuwa unaibeba ukiwa umemaliza kutumia dawati hilo. Endapo utasahau USB yako kwa bahati mbaya kwenye Dawati la kujihudumia, VAC itajaribu kukutaarifu na itaharibu vifaa vyovyote ambavyo havijadaiwa ndani ya masaa 48