Fatilia maombi yako

Fuatilia Maombi yako ya Viza

Unaweza kutumia huduma ya 'Fuatilia ombi lako' kwenye tovuti hii ikiwa tu tayari umetuma ombi la visa au pasipoti katika Kituo cha Maombi ya Visa za Kanada na umepokea risiti ya kukiri pamoja na nambari ya kufuatilia. Huduma hii hukupatia taarifa kuhusu eneo ombi/pasipoti yako ilipo sasa, na si hatua halisi ya mchakato wa maombi.

Kumbuka Muhimu: Ikiwa umetuma ombi lako la visa mtandaoni moja kwa moja kwenye tovuti ya IRCC, tafadhali tambua kuwa taarifa inayohusiana na ombi lako la visa inaweza tu kupatikana kutoka kwa tovuti ya IRCC: https://www.canada.ca/en/immigration-refugees-citizenship/services/application/check-status.html

Mara tu unapotuma ombi/pasipoti yako katika Kituo cha Maombi ya Visa za Kanada, unaweza kufuatilia ilipo pasipoti yako kwa kutumia huduma ya "Fuatilia ombi lako" kwenye tovuti hii.

Unaweza kufuatilia pasipoti/nyaraka zako kupitia gumzo la mtandaoni/mtandao/nambari ya usaidizi/barua pepe iliyotolewa hapa chini. Ili kufuatilia pasipoti/nyaraka zako mtandaoni, itabidi uweke nambari ya Kitambulisho cha Ufuatiliaji iliyotajwa kwenye risiti iliyopokelewa kutoka Kituo cha Maombi ya Visa, na Tarehe yako ya Kuzaliwa.

Zifuatazo ni mbinu za kufuatilia maombi yako:

Gharama za Huduma kwa huduma inayotolewa katika VAC

Gharama ya huduma (kwa kila muombaji)Kiasi kwa Dola ya Kanada (na kodi)Kiasi kwa Shilingi za Kitanzania (na kodi)

Nakala

$0.26500.00

Uchapaji

$0.521,000.00

Ujumbe Mfupi wa Simu

$3.00 5,600.00
Website

Tovuti

Bofya hapa
Chat

Usogozi wa Mtandaoni

Bofya hapa
Phone

Namba za huduma kwa wateja

Wasiliana nasi

Unaweza kutumia huduma za ujumbe mfupi za VFS Global ili uwe na taarifa ya maendeleo ya maombi yako. Lakini, huduma hii inapatikana kwa malipo ya ziada. Mara tu Ofisi za Visa ya Kanada wakimaliza kupitia maombi lako, watafanya maamuzi na kubandika visa kwenye pasipoti yako, au watakupatia barua yenye kuelezea kwa nini hukuweza kupewa viza. Ofisi ya Viza za Kanada itarudisha pasipoti yako kwenye Kituo cha Maombi ya Viza za Kanada, na kituo kitakujulisha hali ya ombi lako kwa njia ya mawasiliano utakayopendelea. Mfumo wa Kimtandao wa Ufuatiliaji wa Maombi ya Viza utakujulisha pindi pasipoti yako itakapokuwa tayari kurudishwa. Itakubidi ufike katika Kituo cha Maombi ya Viza za Kanada kupokea pasipoti yako.